Ruto Kutoa Hati Miliki 200,000 kwa Wakazi wa Pwani
By Katiwa Maneeno @peopleandlifepaper MOMBASA — Zaidi ya hati miliki 200,000 zinatarajiwa kutolewa kwa wakazi wa Pwani wakati wa ziara ya Rais William Ruto katika eneo hilo itakayoanza Ijumaa ijayo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nixon Korir, alisema Serikali imepiga hatua katika kushughulikia masuala ya umiliki wa ardhi katika kaunti za Mombasa, Kwale, Kilifi na Tana River. Korir alisema Serikali inaendelea kutatua migogoro ya ardhi na kukamilisha mipango ya makazi ili kuwawezesha wakazi kupata hati miliki halali. Hata hivyo, baadhi ya maeneo bado yanakabiliwa na changamoto, ikiwemo hati za upangishaji ardhi zilizokwisha muda na madai yanayokinzana ya umiliki. Korir alizugumza hayo wakati wa mkutano wa Kamati ya ardhi uliofanyika mjini Mombasa tarehe 21 Sept 2026. Mkutano ambao ulizungumzia maswala ya umiliki ,uuzaji na hatimiliki za ardhi . Kamati hio ulizungumzia zaidi maswala ya mabwenyeye wenye mashamba makubwa mkoani pwani huku wakisisitiza nia ya serikali kununua masham...